Jumatatu, 25 Mei 2015

TENGENEZA SCRIPT

JINSI YA KUANDIKA MISWADA
(SCRIPT) YA FILAMU
Unapoandika mswada[script] kuna vitu vitatu vya
msingi kuzingatia:
• Muhusika (character)
• Muundo (plot)
• Dhamira (theme)
1. TUKIMZUNGUMZIE MUHUSIKA KWANZA
Mswada wa filamu una sehemu kuu nne ambazo
kila mwandishi lazima azipitie ili mswada wake
uwe nzuri, kwanza kabisa ni hadithi yenyewe
kwa ujumla yaani lazima iwe na wazo [idea]
kamili kwenye kila mstari mmoja inayoonyesha
nani ni muhusika mkuu na nini malengo yake
ambayo katika hadithi [story] yako amepanga
kuyafikia,kwa mfano unaweza kuwa na hadithi
[story concept] kuwa Lucy ni msichana mwenye
miaka 21 na malengo yake ni kuja kuwa
mwanasheria ili aweze kumsaidia baba yake
ambaye yupo gerezani miaka kumi sasa kwa
kesi ya kusingiziwa na hadi sasa bado
hajahukumiwa.huyu ni muhusika mkuu wa filamu
yako sasa ili aje afikie malengo yake kuna
vikwazo vingi sana anavyopitia.
Wahusika pia ni hatua [stage] nyingine katika
kuandika mswada[script], hawa ni watu
wanaosaidia hadithi kufikia pale mwandishi
anapotaka ifike,yaani wanaijaza hadithi [story]
na kuwa yenye mvuto.
Wahusika katika filamu wanahitaji, moja ni
vitendo, pili ni malengo tatu wanahitaji
muelekeo, hii ina maana kuwa ni lazima kuwe
na sababu ya kwa nini huyu mhusika anafanya
au kufanyiwa jambo fulani,kwa mfano katika
malengo pale mhusika anapokwama na
kuendelea kuhangaika inasaidia mtazamaji naye
kuhusika katika filamu na inafikia kipindi
mtazamaji sasa anatamani aingie akamsaidie
kwenye hiyo hadithi [story] yako.
unapomshirikisha mtazamaji katika namna moja
au nyingine anafurahia sana filamu hiyo na
kuona kama inamgusa kabisa.
Na ili mhusika mkuu aweze kucheza nafasi yake
vizuri ni lazima awe na wahusika wengine
watakao msaidia au kumpinga yeye.
[Antagonistic]
MUUNDO
Muundo wa hadithi [story] yenyewe pia ni suala
la msingi sana la kuzingatia hapa ,muundo wa
hadithi ndiyo unaoonyesha matukio na uhusiano
baina ya wahusika na nini kinachotokea kwenye
hadirhi [stori] na vile vile inaonyesha nini
kinatokea kwenye hadithi hiyo.
Mtindo wa maneno na vitendo ulivyopangwa
hupangwa vizuri ili kuongeza matukio katika
hadithi.
Muundo kwa kawaida uwa umegawanyika katika
sehemu tatu yaani mwanzo,kati na
mwisho.inategemea na mwandishi mwenyewe
ameamuaje kuna hadithi zinazoanzia mwisho
kwenda mwanzo kama wenzetu wahindi
wafanyavyo katika kiwanda chao walicho kiita
[ BOLLYWOOD] au pengine huanza kati, mwanzo
alafu mwisho au wakati mwingine kwa muundo
wa moja kwa moja yaani mwanzo hadi
mwisho.na vile vile matendo yanaweza kuelezea
hadithi au muhusika anaelezea hadithi hiyo
kama inavyokuwa kwenye riwaya.
Mara zote unapoandika hadithi yako ni lazima
uanze na swali ‘’itakuwaje’’ (what if) na kila
filamu huwa inafuraha na huzuni.
DHAMIRA
Kabla ya kuanza kuandika mswada[script] kuna
maswali unayotakiwa kujiuliza na kutoa majibu
yake ili pale unapoandika uwe na mtiririko mzuri
wenye kuvutia kwa kila atakayesoma hadithi au
tizama filamu yako,mfano wa maswali yaliyo ya
wazi kabisa ni kama yafuatayo;
• Muhusika mkuu wako ni yupi [who is your
main character?]
[What is he/she trying to accomplish?]
• Kuna vizuizi gani anavyopata kutoka kwa
muhusika mwingine? ( who is trying to stop her/
him )
• Kitatokea nini endapo atashindwa kufikia
malengo yake? (What happens if she/he fails?)
• Scene inaanzia wapi na scene itaishia wapi?
[Where do I start the scene and end the scene?]
• Je kuna uhusiano wowote kati ya tukio [scene]
moja na nyingine? [Is there any relationshinship
between one scene and another?]
• Je matukio [scene] yako yame pooza [flat] na
kujirudia rudia,na kutokuwa na mvuto?
• Na je!mtazamaji atafurahia kuangalia filamu?
Hayo ni maswali ya msingi sana na kama
mwandishi akiyazingatia mwisho wa siku
ataandika mswada [script] mzuri na kila mtu
atavutiwa nao.
Vile vile katika uandishi wa mswada [script]
ubunifu ni kitu cha msingi sana cha kuzingatia,
na ubunifu huo unapaswa uendane na mlolongo
wa hadithi yako na kukumbuka hasa nini uweke
kwenye hadithi yako na nini usiweke kwenye
mswada huo .
Mbali na hayo pia unapoandika mswada [script]
jambo la msingi katika hadithi ni mgogano
(conflict)
Unapoandika msawda [script] wako mfano
kuhusu kijana anayetaka kuwa dokta hivyo
anamuomba baba yake amsaidie fedha zitakazo
msaidia katika masomo yake na anamatarajio
makubwa sana ya kupata msaada kutoka kwa
baba yake matokeo yake baba anamkatalia na
kumwambia fedha aliyonayo ni ya kumsomesha
uhasibu ili aje asimamie miradi ya familia hapo
tayari kunatokea mgongano baina ya baba na
mtoto,hivyo basi unashauriwa kuonyesha
mgongano mapema iwezekanavyo,kama
nilivyosema mwanzo,mgongano ndiyo unabeba
hadithi,usipoweka mgongano hadithi haiwezi
kuvutia,kama nilivyoonyesha huo mfano hapo juu
endapo baba angempa ada na kusoma
akamaliza na kuwa daktari hakuna kitu ambacho
kingeweza kumvutia mtazamaji.Hivyo hakikisha
mgogoro unakuwa mkubwa kabla ya kufikia
kwenye suluhisho.kwa kutumia mfano wa juu
huyu kijana anasimamia msimamo wake na
baba nae anasisitiza mwanae asome uhasibu
,mwisho baba anamfukuza mtoto wake
nyumbani ,anaondoka na kuanza kuishi maisha
ya kutanga tanga ambayo ni bora angekubali
matakwa ya baba yake.
Ni vizuri sana mgogoro ukipata ufumbuzi
ambapo ndiyo hatua ya mwisho kabisa ya
hadithi na katika mfano wetu huo huo kijana
anaondoka na kwenda mbali akiwa kule maisha
yanambana sana na kuamua kurudi nyumbani
kuongea na baba yake kuwa yupo tayari kwenda
kusoma uhasibu lakini akiwa na nia akipewa tu
ada anaenda kusoma udaktari anafika nyumbani
na kuongea na baba yake anayemsamehe na
kuahidi kumpa ada lakini kwa bahati mbaya siku
inayofuatia baba anadondoka bafuni na
kupoteza maisha,linakua pigo jingine kwa kijana
hivyo anashindwa kwenda kusoma kwa muda
huo inabidi asimamie miradi ya baba yake na
baada ya miaka mitatu mbele anafanikiwa na
kwenda kusoma udaktari.
Huu ni mfano mmoja wapo wa mgogoro ingawa
kuna migogoro mingine ambayo inaweza kuwa
wa nafsi (internal conflict),mtu na mtu kama
huu wa baba na mtoto,ipo mingine ya kijamii na
mtu na jamii.
Hadi kufikia mwisho hadithi au mswada[script]
inatakiwa kuwa katika mfumo huu kama mchoro
unavyoonyesha.
1.MWANZO[START]
2.MIGOGORO[CONFLICT]
3.SHULUHISHO[RESOLUTION]
BEGINNING/MWANZO END/MWISHO
Na vile vile kuna software nyingi zinazoweza
kusaidia katika kuandika script mfano final
cut,celtix na nyingine nyingi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni